STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, November 30, 2013

Zanzibar Heroes kuvuna nini leo kwa Ethiopia, Kili Stars kesho!


Zanzibar Heroes wanaotarajiwa kuvaana na Ethiopia leo katika Chalenji
WAKATI mabingwa watetezi Uganda jana wakianza vyema mbio zake za kuwania taji la 14 la Kombe la Chakenji kwa kuilaza Rwanda bao 1-0, huku Sudan ikiisasambua Eritrea kw amabao 3-0, wawakilishi wa Tanzania upande wa visiwani, Zanzibar Heroes leo inatarajiwa kushuka uwanjani kuumana na Ethiopia.
Hilo ni pambano la pili na washindi wa tatu wa michuano iliyopita baada ya awali kuanza mechi za michuano hiyo kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sudan Kusini.
Zanzibar Heroes ambayo inanolewa na kocha Seif Bausi na inayoundwa na wachezaji wengine chipukizi italazimika kupata ushindi wa leo mbele ya Ethiopia iliyoanza na sare ya 1-1 dhidi ya wenyeji Kenya ili kuweka hai nafasi ya kutinga robo fainali.
Ethiopia waliokuwa katika kinyang'anyiro cha kuwania kutinga Fainali za Kombe la Dunia 2014 na kutolewa na Nigeria, siyo timu ya kubeza, hivyo vijana wa Zanzibar Heroes wanapaswa kuwa makini katika mechi hiyo ya leo iwapo inataka kudhihirisha kuwa haikuiotea Sudan Kusini walipoilaza mechi iliyopita.
Mechi nyingine inayochezwa leo kwenye mfululizo wa michuano hiyo itakayofikia tamati Desemba 12 ni kati ya Harambee Stars dhidi ya Sudan Kusini.
Kikoi cha Kilimanjaro kitakachoshuka dimbani kesho dhidi ya Somalia
Wawakilishi wa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars iliyoanza kwa sare ya 1-1 na mabingwa wa zamani wa Afrika, Zambia yenyewe itashuka kesho kupepetana na Somalia kabla ya wiki ijayo kumalizia mechi zake za kundi B dhidi ya Burundi, ambapo wenyewe kesho wataumana na Zambia 'Chipolopolo'.

No comments:

Post a Comment