STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, November 30, 2013

Baada ya kutemeshwa Uhai Cup, Azam sasa wajifariji


Baadhi ya nyota wa Azam waliopo Kilimnajrao Stars, Murad, Mao na Kussi wakikabana na Mari Kiemba wa Simba

LICHA ya kuyaaga mashindano ya uhai Cup katika ngazi ya nusu fainali baada ya kufungwa 1-0 na Coastal Union, wanafainali wa Uhai Cup mwaka jana ambapo kombe lilichukuliwa na Azam Academy, bado Azam Academy imekuwa timu ya mfano na kujivunia baada ya kutoa wachezaji wanne kwenye kikosi cha timu ya taifa Kilimanjaro Stars inayoshiriki mashindano ya GoTV CECAFA Challenge Cup

Huenda kutolewa kwa Azam Academy kumechangiwa na kukosekana kwa nyota hao ambao haiyumkini uwepo wao ungeisaidia sana Azam Academy, lakini uongozi wa Azam FC bado unajivunia kikosi chake cha timu ya vijana.

Uongozi wa Azam FC haumlaumu kocha kim Poulsen kwa kuchukua wachezaji wake bali unajisikia faraja kuona vijana wake wakipata nafasi ya kuwakilisha nchi kwani hilo ndilo lengo kuu la Azam FC (Mapinduzi ya Soka la Tanzania)

Aishi Salum Manula, mmoja wa magolikipa bora nchini na mlinda mlango namba mbili wa kikosi cha kwanza cha Azam FC anatoka kwenye academy hii na hii ni faida zaidi ya kutwaa Uhai Cup.

Lakini si Aishi pekee, Farid Mussa Malik na mchezaji bora wa vijana wa Gazeti la Mwanaspoti Joseph Kimwaga ambaye goli lake la dakika ya 90 lilitosha kuipa ushindi Azam FC dhidi ya Yanga wamo kwenye kikosi cha timu ya taifa na hili linaifanya Academy ya Azam FC iwe na maaana zaidi ya academy nyingize zilizopo nchini.

Katika kikosi kilichopo Nairobi, kocha Kim Paulsen amemjumuisha Ismail Adam Gambo kikosini na kufanya wachezaji kutoka Azam Academy kufika wanne.

Lakini utasema nini kuhusu Braison Raphael? Huyu ni zaidi ya lulu kwenye soka la Tanzania, moyo wake wa kupambana, ushujaa wa kujitolea na safari zake kwenye dimba la soka kunamfanya awe mchezaji wa kipekee… ni dhahiri Braison Raphale atapaa kwenda kikosi cha kwanza hivi karibuni kama ilivyo kwa Gardian Michale ambae kama ilivyo kwa Braison, wameonesha kiwango kikubwa sana.

Wachezaji wengine walioonesha kiwango kikubwa kwenye mashindano haya ni, beki wa kati Yaruk Dizana na winga teleza mwenye uwezo mkubwa na kuuchezea mpira Erick Haule….

Wawili hawa watapata mafanikio makubwa sana kama watapata nafasi ya kujiendeleza.

Azam Academy pia inajivunia uwepo wa Mudathir Yahya kwenye kikosi cha kwanza ambaye ameungana na Samih Haji Nuhu na Himid Mao Mkamy ambao walipandishwa miaka mitatu iliyopita.

Kutokana na hayo licha ya Azam FC kusononeka kutokana na kutolewa kwenye hatua ya nusu fainali za Uhai Cup, lakini mafanikio haya ya kuzalisha vipaji ambayo vimeweza kupevuka na kuwa na manufaa ndani ya muda mfupi unatoa faraja na kuonesha dira ya mafanikio.


AZAM FC

No comments:

Post a Comment