STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, November 30, 2013

Fainali za EBSS kipwanipwani leo Escape 2

http://api.ning.com/files/Vkr5AOZtf8IZ*LagrRC25iuMgDMtqJBcY*2rC84HA-D2knVsJ1IRqqnYPVSh4FaKmVYZCkbH2bxVmkvhjegztCTP06*wPYSO/EBSSFINALEPROMOPOSTER1.jpg

FAINALI ya shindano la kusaka vipaji vya kuimba la Epiq Bongo Star Search ambalo linafanyika leo katika ukumbi wa Escape 2 jijini Dar es Salaam litapambwa pamoja na burudani nyingine, wakali wa miondoko ya pwani wanaotamba sasa nchini Snura na Shaa.
Snura amejizolea umaarufu nchi nzima kutokana na singo yake ya 'Majanga' katika kipindi ambacho Shaa anakuja juu kutokana na wimbo wake mpya wa 'Sugua Gaga' ambazo zote zinachezeka kwa kuzungusha kiuno zaidi.
Akizungumza na MICHARAZO jana, jaji mkuu wa shindano hilo Ritta Poulsen alisema mbali ya Snura na Shaa, wasanii wengine watakaotoa burdani ni Barnaba, Komandoo, Msechu na 'live' bendi.
Alisema safari hii onyesho hilo litakuwa la aina yake kutokana na kujiandaa vya kutosha ili kuhakikisha wanawapa burudani nzuri mashabiki wa shindano hilo ambalo hufanyika kila mwaka.
Mshindi atazawadiwa sh. milioni 50 pamoja na kuingia mkataba wa mwaka mmoja na wadhamini wakuu wa shindano hilo, kampuni ya simu za mkononi Zantel, alisema Rita.
Mshindi huyo pia atasaini mkataba wa jinsi gani atazitumia fedha za zawadi ambazo atapewa na waandaaji wa shindano hilo, alisema Rita ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Bench Mark.
"Tumeamua kufanya hivyo ili kuhakikisha mshindi anazitumia vizuri fedha ambazo atazipata mara baada ya kuibuka mshindi katika shindano hilo," alisema.
Naye Barnaba alisema amejiandaa kutoa burudani safi kwa mashabiki watakahudhuria onyesho hilo, ikiwemo kutambulisha nyimbo yake mpya ya 'Jasho la Mnyonge'.

No comments:

Post a Comment