STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, December 13, 2013

Neymar achekelea kuweka heshima Ulaya mapema zaidi

http://bostonherald.com/sites/default/files/styles/full/public/media/ap/d7a9ff3209aa48e190d014ef0569a8cf.jpg?c=612f6677417bc1fda3fcf6c08e08968f
Neymar akishangilia moja ya mabao yake matatu yaliyoizamisha Celtic juzi
BARCELONA, Hispania
NEYMAR amesema ameweka heshima Ulaya baada 'hat-trick' yake aliyofunga kuisaidia Barcelona kushinda 6-1 dhidi ya Celtic.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil alifunga magoli matatu ndani ya dakika 13 wakati Bara walipomaliza hatua ya makundi kwa ushindi mnono, huku Gerard Pique, Pedro na Cristian Tello wakifunga mabao mengine.
Barca waliingia katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Nou Camp wakiwa wamepoteza mechi mbili katika ya tatu zilizopita na Neymar alifarijika kwamba kikosi cha kocha Gerardo Martino kimerejea kushinda tena.
"Nina furaha - siyo tu kwa kufunga magoli matatu kwenye Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, ila pia kwa timu kushinda," alikaririwa na gazeti la Marca akisema.
"Sikuwa katika presha, lakini nilitaka kuweka heshima. Jambo muhimu ni kwamba tumeweza kuzipiku mechi zile mbili tulizopoteza na sasa ni lazima tubadili mitazamo yetu na kufikiria La Liga. "
Alipoulizwa kama anapenda kucheza katikati kuliko pembeni, alikataa kutoa maoni yake katika hilo, akisema anachohitaji ni kucheza tu.
"Napemda kucheza, sijali ni katikati ama pembeni," Neymar aliongeza.
Mechi ijayo ya Barca itakuwa ni ugenini dhidi ya timu ngumu ya Villarreal kesho baada ya kumaliza wakiwa vinara wa Kundi H la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Na tofauti ya mabao katika kipigo cha kwenye Uwanja wa Nou Camp imeifikia rekodi ya kufungwa 5-0 dhidi ya Artmedia Bratislava katika iliyokuwa mechi ya kwanza madarakani kwa kocha wa zamai Gordon Strachan mwaka 2005.
Celtic waliingia katika mechi hiyo wakiwa wamefunga jumla ya magoli 12 na hawajaruhusu hata moja katika mechi zao mbili za ligi zilizopita, wakati Barcelona walikuwa wamekula vipigo kutoka kwa Ajax na Athletic Bilbao.
Lakini Barca waliokuwa katika kiwango chao cha juu waliishushia Celtic kipigo chao cha 25 katika mechi 27 za ugenini za Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

No comments:

Post a Comment