STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, December 13, 2013

Offside Trick sasa watoa Talaka hadharani

Mmoja wa wanaounda kundi la Offside Trick, Hammer Q
KUNDI maarufu la miondoko nya mduara, Offside Trick la visiwani Zanzibar, limeachia wimbo mpya uitwao 'Talaka' ikiwa ni siku chache tangu waachie video ya wimbo wao wa 'Nipe Nikupe waliomshirikisha Mzee Yusuf.
Mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo, Hussein Mohammed 'Hammer Q', aliiambia MICHARAZO kuwa wameamua kutoa wimbo huo mpya kama zawadi kwa mashabiki wao katika kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2014.
Hammer Q alisema wimbo huo kama zilivyo nyimbo zao nyingine zipo katika miondoko hiyo ya mduara na wanafanya mipango kurekodi video yake.
"Baada ya kuachia video ya 'Nipe NIkupe' tuliyoimba na Mzee Yusuf, tumeachia wimbo mwingine mpya uitwao 'Talaka' ambao tumeimba sisi wenyewe Offsiede Trick bila kumshirikisha mtu wakati tukijipanga kufanya video yake," alisema Hammer.
Kundi hilo la Offside Trick linaundwa na wasanii wawili Said Amdani 'Lil Ghetto' na Hammer Q aliyeziba nafasi ya Mudi Chriss aliyepo masomoni.

No comments:

Post a Comment