STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, March 18, 2014

Jennifer Mgendi ana Shelina na Bonny Mwaitege, Bahati Bukuku

BAADA ya kitambo kirefu tangu alipoachia filamu yake ya mwisho ya 'Chai Moto' muimbaji mahiri wa muziki wa Injili nchini, Jennfer Mgendi anatarajiwa kuibuka na kazi mpya iitwayo 'Shelina'.
Akizungumza na MICHARAZO, Mgendi alisema filamu hiyo itakayozungumzia changamoto wanazopata watoto wa kike na jinsi imani ya Mungu inavyoweza kuleta ufumbuzi wa changamoto hizo itawashirikisha wasanii mbalimbali wa filamu na muziki wa Injili nchini.
Mgendi, ambaye anaendelea kutamba kwa sasa na albamu yake mpya ya 'Hongera Yesu' alisema miongoni mwa wasanii watakayoicheza filamu hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi Juni mwaka huu ni pamoja na Bahati Bukuku, Bonny Mwaitege, Bibi Esther, Christina Matai na wengineo.
"Nipo katiuka hatua ya mwisho kabla ya kuanza kushuti ila itafahamika kwa jina la 'Shelina' na itawashirikisha wasanii kadhaa nyota wa filamu na muziki wa Injili nchini, akiwamo Bahati Bukuku, Boniface Mwaitege," alisema.
Kabla ya filamu hiyo, Mgendi alishatoa filamu za 'Joto la Roho', 'Pigo la Faraja', 'Teke la Mama' na 'Chai Moto' inayoendelea kutamba kwa sasa sokoni

No comments:

Post a Comment