TIMU ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania
kutoka Kituo cha Mwanza imeondoka leo (Machi 26 mwaka huu) kwenda Brazil
kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia kwa Watoto wa Mitaani.
John Kadutu ambaye ni mjumbe wa Bodi
ya kituo hicho, na pia mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) akiwakilisha klabu za Mkoa wa Mwanza ndiye kiongozi wa msafara
wa timu hiyo ya Tanzania.
Michuano hiyo ya siku 10
inayoshirikisha watoto wa mitaa (wavulana na wasichana) inaanza keshokutwa
(Machi 28 mwaka huu). Nchi 19 zinashiriki michuano hiyo itakayofanyika katika
Jiji la Rio de Janeiro.
Mbali ya Tanzania, nchi nyingine
zinazoshiriki michuano hiyo kwa upande wa wavulana ni Argentina, Burundi,
India, Kenya, Liberia, Marekani, Mauritius, Misri na Pakistan. Kwa wasichana ni
Afrika Kusini, Brazil, El Salvador, Indonesia, Msumbiji, Nicaragua,
Philippines, Uingereza na Zimbabwe.
Mwaka 2010 mashindano hayo
yalifanyika Durban, Afrika Kusini ambapo pia Tanzania ilishiriki.
No comments:
Post a Comment