KWA HABARI ZA BURUDANI, MICHEZO NA MATUKIO MBALIMBALI
STRIKA
USILIKOSE
Tuesday, March 25, 2014
Kamati ya Sheria TFF kukutana juu ya Katiba
Rais wa TFF, Jamal Malinzi
KAMATI
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
inatarajia kukutana mwishoni mwa wiki kupitia taarifa ya utekelezaji wa
agizo la wanachama kurekebisha katiba zao.TFF
ilitoa agizo kwa wanachama wetu kufanyia marekebisho katiba ikiwemo
kuingiza Kamati ya Maadili. Mwisho wa utekelezaji wa agizo hilo ulikuwa
Machi 20 mwaka huu.
Hivyo,
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itapokea taarifa ya utekelezaji
wa agizo hilo kutoka kwa Sekretarieti, na baadaye kutoa mwongozo wa
hatua inayofuata.
No comments:
Post a Comment