Tp Mazembe |
Al Ahly |
Kundi B la michuano hiyo limezikutanisha timu za waarabu watupu, Esperance na C.S Sfaxien za Tunisia E.S Setif ya Algeria na Ahly Benghazi ya Libya.
Katika droo iliyotolewa inaonyesha michezo za makundi hayo zitaanza kuchezwa kati ya Mei 16 na 18 na 23 na 25, Juni 6 na 8, Julai 25 na 27, Agosti 8 na 10 na 22 na 24 huku timu zitakazoshika nafasi mbili za juu kwenye makundi zikisonga Nusu Fainali.
Wakati huo huo ratiba ya makundi kwa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika nayo imepangwa ambapo wababe wa Yanga, Al Ahly ya Misri imepangwa kundi B linalotajwa kama la kifo.
Kundi hilo linajumuisha timu za Sewe Sport ya Ivory Coast, Etoile du Sahel ya Tunisia na Nkana Red Devils ya Zambia.
Kundi A lenyewe lina timu za Coton Sport ya Cameroon, ASEC Mimosas ya Ivory Coast, AS Real ya Mali na AC Leopards ya Kongo Brazzaville.
Mechi za michuano hiyo zinatarajiwa kuchezwa kuanzia kati ya Mei 16 na 18 na Juni 23 na 25, Juni 6 na 8, Julai 25 na 27, Agosti 8 na 10 na 22-24 na washindi wawili wa kila kundi watasonga Nusu Fainali.
Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika
Kundi A: TP Mazembe (DRC), Al-Hilal (Sudan), Zamalek (Misri) na AS Vita (DRC)
Kundi B: Esperance (Tunisia), CS Sfaxien (Tunisia), Entente Setif (Algeria) na Al-Ahly Benghazi (Libya).
Makundi Kombe la Shirikisho Afrika:
Kundi A: Coton Sport (Cameroon), ASEC Mimosa (Ivory Coast), AS Real Bamako (Mali) na AC Leopards (Congo)
Kundi B: Al Ahly (Misri), Sewe Sport (Ivory Coast) Etoile du Sahel (Tunisia) na Nkana Red Devils (Zambia)
No comments:
Post a Comment