STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, June 11, 2014

Abid Kassim 'Babi' azidi kuwatesa makipa Malaysia

KIUNGO Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Kassim 'Babi' anayekipiga katika timu ya UiTM ya Malaysia anazidi kung'ara baada ya kufanikiwa kufikisha mabao matano katika Ligi Kuu ya nchi hiyo.
Idadi hiyo imemfanya nyota huyo wa zamani wa Yanga, Mtibwa Sugar, Azam na Taifa Stars kushika nafasi ya pili ndani ya klabu yake  nyuma ya Mnigeria Obi Ikechukwu Charles mwenye mabao nane.
Aidha ushirikiano wa Babi ambaye pia ni nahodha wa UiTM umeiwezesha timu hito kuchupa toka maeneo ya mkiani na kushika nafasi ya saba ikijikusanyia pointi 20 kutokana na mechi 18.
Akizungumza na MICHARAZO toka Malaysia, nyota huyo alisema timu yao imechupa hadi nafasi hiyo baada ya jana kuilaza Perlis kwa mabao 2-0.
"Nashukuru ndugu yangu mpaka sasa nimefikisha goli 5 katika Ligi Kuu nikiwa ni mfungaji wa pili ndani ya klabu nyuma ya Mnigeria Obi Ikechukwu mwenye mabao nane, na nipo nafasi ya 12 kwenye msimamo wa wafungaji wa ligi hiyo orodha inayoongozwa na mzawa Edward Junior Wilson wa klabu ya Felda United mwenye mabao 17," alisema.
Babi aliyewahi kuzichezea pia KMKM na klabu ya DT Dong ya Vietnam alisema ligi ya nchi hiyo ni ngumu, ila wanashukuru timu yao inazidi kuimarika na kukamata nafasi ya 7 na pointi zao 20 na siku ya Ijumaa watashuka dimbani kuvaaana na DRB-Hicom  katika pambano la ugenini litakalochezwa kwenye uwanja wa Hang Jebat uliopo mji wa Malacca.

No comments:

Post a Comment