STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, June 10, 2014

Hatimaye yametimia, AC Milan yamtimua Seedorf

HATIMAYE klabu ya AC Milan ya Italia imemtimua kocha wake Clarence Seedorf na kumuajiri Filippo Inzaghi kuchukua nafasi hiyo kama tetesi zilizokuwapo kwa wiki mbili zilizopita.
Seedorf raia wa Uholanzi aliteuliwa kuinoa timu hiyo Januari mwaka huu kuchukua nafasi ya Massimiliano Allegri aliyetimuliwa. 
Licha ya kuingoza timu hiyo kukaribia kupata nafasi ya kucheza michuano ya Europa League, ilitegemewa Seedorf kuachia manyanga kutokana na kushindwa kuelewana na Rais Silvio Berlusconi pamoja na ofisa mkuu Adriano Galliani. 
Klabu hiyo sasa imethibitisha kumtimua kiungo huyo wa zamani wa timu hiyo na kumchagua Inzaghi kuziba nafasi yake baada ya kuingoza vyema timu ya vijana chini ya umri wa miaka 19 aliyokuwa akiifundisha.

No comments:

Post a Comment