STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, June 10, 2014

Kanali Mwanakatwe kuzikwa leo mjini Babati

Rais Jakay Kikwete akitia saini kitambu cha maombolezo cha Kanali Ally Mwanakatwe anayetarajiwa kuzikwa leo kwao mjini Babati, Manyara
MAZISHI ya aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakati huo likiitwa FAT, Kanali mstaafu Ali Hassan Mwanakatwe yanafanyika leo (Juni 10 mwaka huu) Magugu, Babati mkoani Manyara.
Kanali Mwanakatwe alifariki dunia Juni 7 mwaka huu katika Hospitali Kuu ya Jeshi (GMH) Lugalo jijini Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu baada ya kuanguka bafuni nyumbani kwake Mbezi Beach.

TFF imetoa ubani wa sh. 500,000 kwa familia ya marehemu Kanali Mwanakatwe, na katika maziko hayo inawakilishwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Kanda ya Arusha na Manyara, Omari Walii.

No comments:

Post a Comment