STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, June 10, 2014

KOcha mpya Barca afanyiwa upasuaji

MENEJA wa klabu ya Barcelona, Luis Enrique anaendelea vyema baada kufanyiwa upasuaji wa wenye mafanikio wa kidole tumbo. 
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 44 alikimbizwa hospitali Jumatatu baada ya kupata maumivu makali kabla ya vipimo kugundua tatizo lake. 
Taarifa iliyotolewa katika mtandao wa klabu hiyo imedai kuwa upasuaji huo uliofanyika leo umekuwa na mafanikio na kocha huyo anatarajiwa kuruhusiwa hospitali ndani siku chache zijazo. 
Kiungo huyo wa zamani ambaye aliichezea Barcelona kati ya mwaka 1996 na 2004 alitajwa kuchukua nafasi ya kocha Gerardo Martino Mei mwaka huu.

No comments:

Post a Comment