STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, June 10, 2014

Inauma!: Wahubiri wa Kiislam Kenya wazidi kuteketezwa mwingine auwawa

Mwenyekiti wa Baraza la Maimamu na Wahubiri (CIPK) Sheikh Mohammed Idriss (kulia) enzi za uhai wake akiwa na Afisa wa baraza hilo Sheikh Hassan Suleiman
VIFO vya Wahubiri wa Kiislam vimeendelea kujiri nchini Kenya baada ya mhubiri mwingine wa dini hio kuuwawa mjini Mombasa kuendeleza mfululizo wa vifo vya viongozi wa kidini nchini humo.
Sheikh Mohammed Idris, ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Maimamu na Wahubiri nchini Kenya, aliuawa karibu na msikiti ulio karibu na nyumba yake na watu wasiojulikana kwa kumiminiwa risasi.
Duru zinasema kwa alikuwa amepokea vitisho kutoka kwa vijana  wenye itikadi kali za kidini na tayari alikuwa ameelezea hofu juu ya maisha yake.
Wahubiri kadhaa mashuhuri wameuawa katika hali ya kutatanisha katika miaka ya hivi karibuni.
Wengine waliuawa kwa madai ya kuwa na uhusiano wa karibu na kundi la wanamgambo la al-Shabaab huku wafuasi wao wakiilaumu serikali kwa mauaji yao, madai ambayo serikali imakenusha.
Marahemu Idris alikuwa ameitaka serikali kukabiliana na baadhi ya watu wenye itikadi kali za kidini ndani ya msikiti hali ambayo ilisababisha baadhi ya waumini kumuita msaliti.
Kifo cha muhibri huyo kimekuja huku kukiwa na mfululizo wa vifo vya vioingozi wa kidini wa kiislam na kuleta hofu kubwa, sambamba na kile kinacjhoelezwa kuchochea ulipizaji kisasi unaofanywa na kundi la Al Shaabab linaloripotriwa kila mara likilipua mabomu nchini humo na hasa mjini Mombasa.

No comments:

Post a Comment