Na Boniface Wambura
WACHEZAJI wa Tanzania walioko
Uholanzi, Dickson Ambundo na Shiza Yahya wameanza kuonekana muda na
waandaaji ya mashindano ya AEGON Copa Amsterdam.
Kwa mujibu wa wakala wa wachezaji
wa Uholanzi, Denis Kadito, AEGON Copa Amsterdam ni mashindano ya
kimataifa yanayoshirikisha timu kubwa kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni
kwa wachezaji wa miaka chini ya 19.
Kwa Uholanzi, Ajax Amsterdam huwa
lazima washiriki, na pia huwa kuna timu ya ridhaa inayotengenezwa kwa
kuchagua “best talent” kutoka Uholanzi. Mchujo wa wachezaji hao
kutengeneza timu ya kombaini, ulianza na wachezaji wasiopungua 1,000.
Kombaini hiyo inaitwa Men United
na inafundishwa na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi, Ronald
de Boer. Ronald e Boer ni pacha wa kocha wa Ajax (First team).
Enzi
akiwa Tnazania: Beki wa Falcon ya Zanzibar Faki Hamad akiwa amemiliki
mpira huku Dickson Ambundo wa Serengeti boys akitafuta mbinu za kumpora.
Ronald de Boer pia ni kocha wa
wachezaji washambuliaji wa Ajax. Shiza na Ambundo waliingizwa kwenye
mchujo na wakafanya vizuri, mwishoni wakaitwa kwenye timu ya wachezaji
18 waliotengeneza timu ya Men United. Hii ni mara ya kwanza wachezaji
wasio Waholanzi kuingizwa katika timu hiyo.
Mashindano ya Copa Amsterdam
yameanza juzi (Juni 8 mwaka huu) na yanaisha kesho (Juni 11 mwaka huu.
Katika mashindano hayo kuna makundi mawili. Kundi A ni AFC Ajax
(Amsterdam), Ajax Cape Town ( Afrika Kusini), Fluminense (Brazil),
Hamburg SV (Ujerumani) wakati B ni Men United, Panathinaikos (Ugiriki),
FC Aerbin (China) na Cruizero (Brazil).
Shiza na Ambundo wamecheza mechi
zote tatu. Shiza amekuwa akicheza namba tatu wakati Ambundo anapiga
namba tisa, saba na kumi na moja.
No comments:
Post a Comment