STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, July 19, 2014

Pacquiao kuzipiga na Chris Algieri

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg893Gr1QfgTI6wsqE0zCvIUweOOMP-5aNTy5PpKPKp8iwEAwUDWdOAz48TAB8Rn4-LmlFt2mvdw_Um8VpEclGO8hM08oW9Dk5gS9MDvzrSiAgl05r0cGmsdQRn3a0UKyfERey7WO1AJgo/s1600/manny+pacquiao.jpg
Manny Pacquiao
http://fightnews.ru/files/u12355/algieri_01_0.jpg
Chris Algieri
BONDIA Mfilipino Manny Pacquiao (35) atarejea ulingoni Nov. 22 kutetea taji lake la World Boxing Organisation (WBO) uzani wa welterweight dhidi ya bondia wa Marekani ambaye hajawahi kupoteza pambano Chris Algieri litakalofanyika Macau, promota wake Bob Arum amesema.
Ukumbi wa Venetian Macao, ambao Pacquiao mwenye rekodi ya kushinda mapambano 56 kupigwa matano na sare 2 alipata ushindi wa pointi dhidi ya Bondia Mmarekani Brandon Rios Novemba mwaka jana, ndiyo utakaofanyikia pambano hilo.
Aprili mwaka huu, Pacquiao alipata ushindi wa pointi dhidi ya Timothy Bradley na kutetea taji lake la WBO welterweight na kulipa kisasi cha kupigwa kiutata dhidi ya Mmarekani huyo Juni 2012.
"Tumesaini dili. Kwa upande wangu, halikuwa dili gumu hata kidogo," Arum aliambia ESPN.com.
Algieri (30), ambaye ni mpiganaji wa 'kick-boxing', ana rekodi ya kupigana mapambano 20 na kushinda yote na alitwaa taji la WBO light-welterweight mwezi uliopita kwa pointi dhidi ya Mrusi Ruslan Provodnikov

No comments:

Post a Comment