STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, July 19, 2014

Romelu Lukaku kutua jumla Goodson Park

http://worldsoccertalk.com/wp-content/uploads/2013/10/romelu-lukaku.png
KLABU ya Everton inajiandaa kumrejesha tena klabuni mshambuliaji wake nyota Romelu Lukaku alioyekuwa akiichezea timu hiyo kwa mkopo toka Chelsea baada ya dili lake la kwenda kujiunga Atletico Madrid kuota mbawa.
Mbelgiji huyo ni mshambuliaji chaguo la kwanza la kocha Roberto Martinez  majira haya ya kiangazi na anatarajia kukamilisha usajili wake ndani ya saa 48 zijazo.
Martinez, aliyekuwa anamfikiria Demba Ba kama mbadala wa Lukaku, ila hakukubaliana na mshahara aliodai wa paundi elfu 80 kwa wiki, na sasa anataka kumshawishi mbelgiji mwenye miaka 21 kumwaga wino katika kikosi chake cha msimu ujao.
Inafahamika kuwa maandalizi makubwa ya kumrudisha Everton yamekamilika baada ya kurejea kutoka Austria walipoweka kambi.
Lukaku alikuwa anatarajia kusaini Atletico Madrid, lakini kwa bahati mbaya ikawa tofauti kwasababu hakuwa chaguo la kwanza la kocha Diego Simeone.
Wolfsburg  pia walionesha nia kubwa ya kumsajili kama ilivyokuwa kwa Tottenham, lakini Lukaku alifurahia maisha  Goodison na anapenda kuendelea kuisaidia klabu hiyo mpaka kufuzu ligi ya mabingwa.
Martinez pia amefanya mazungumzo ya kumrudisha mchezaji aliyekuwa kwa mkopo, Monaco, Lacina Traore sambamba na kuzungumza na kiungo wa Bosnia ,Muhamed Besic, mwenye miaka 21, anayekipiga klabu ya Ferencvaros.

No comments:

Post a Comment