STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, July 19, 2014

Hatari! Kijana aua mtoto na kula ubongo wake


Askari kanzu wa kituo cha Polisi Himo wakiwa wamemkamata Lawrence Mramba anayetuhumiwa kumuua mtoto wa miaka 9 na kula ubongo wake. PICHA | DIONIS NYATO.

Moshi.  

MKAZI mmoja wa Moshi amemuua mwanafunzi wa darasa la 3 kule Samanga leo na kisha 'kula ubongo' wa mtoto huyo katika tukio la kutisha lililostua wakazi wa mji huu.

Kijana huyu aliyefahamika kwa jina la Lawrence Mramba, 20, alimshambulia mtoto huyo mwenye umri wa miaka 9 kwa panga wakati akienda shule mnamo saa 1 asubuhi Ijumaa, akampasua kichwa na kisha akaanza kutafuna ‘vipande vya ubongo wake.’

Mara baada ya kitendo hicho cha kushtusha, Mramba, aliyeonekana kuwa na matatizo ya akili, alianza kujikatakata sehemu zake za siri na wembe, huku akitafuna vipande vya mwili wake mwenyewe, kimoja baada ya kingine.

Baadhi ya mashuhuda wanadai kijana huyo ‘alionyesha kuwa na nguvu za ajabu’, huku wanakijiji wenzake wakishindwa kabisa kumdhibiti.

Wengi walilazimika kuketi kando wakimtazama jinsi anavyojikata wakishindwa kujua cha kufanya.

Iliwabidi polisi waingilie kati sakata hilo na hatimaye wakifanikiwa kumthibiti kijana huyo.

Hata hivyo, Mramba alifariki dunia muda mfupi baadaye katika hospitali ya Kilema wakati akipewa matibabu ya dharura kutokana na kupoteza damu nyingi.

MWANANCHI

No comments:

Post a Comment