STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, July 19, 2014

Yaya Toure akata mzizi wa fitina adai haendi kokote

http://content.mcfc.co.uk/~/media/Images/Shared/Players/Players1213/First%20Team%20Player%20Profiles/Yaya_Toure.ashx?h=700&mh=700&mw=800&w=800LICHA ya awali kuelezwa hafurahii maisha ndani ya Manchester City hasa baada ya kukerwa na viongozi wake kuipuuza sikua yake ya kuzaliwa, Kiungo nyota wa mabingwa hao wa soka wa England, Yaya Toure amesema hana mpango wa kuondoka katika timu hiyo.
Awali kulikuwa na tetesi kwamba mahasimu wa City, Mashetani Wekundu Manchester United walikuwa wakimvizia ili kumnyakua, lakini mchezaji huyo ameweka bayana kwamba atasalia klabuni hapo kwa msimu mwingine ujao.
Toure alinukuliwa na kituo cha Sky Sport kuwa mashabiki wa timu hiyo wamekuwa wema kwake na kwa familia hivyo ameona ni bora abaki kwa ajili yao. 
Vyombo vya habari vimekuwa vikimhusisha kiungo huyo kuhamia katika vilabu mbalimbali toka wakala wake Dimitry Seluk alipoandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kuwa nyota huyo hajatulia. 
Seluk alitoa madai kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast hakupewa utambulisho rasmi na klabu katika siku yake ya kuzaliwa wakati wa safari yao ya Abu Dhabi huku Toure mwenyewe akiunga mkono kauli hiyo. 
Toure amesema kwa sasa mambo yote yako sawa na baada ya tetesi nyingi kuzungumziwa juu yake anajipanga kufanya kitu kwa ajili ya mashabiki. 
Nyota huyo alijiunga na City akitokea Barcelona mwaka 2010 na haraka alijitengenezea jina na kuwa mchezaji tegemeo akiisaidia City Kombe la FA mwaka 2011 na mataji mawili ya Ligi Kuu mwaka 2012 na 2014.

No comments:

Post a Comment