STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, July 19, 2014

Phillip Lahm atangaza kustaafu soka baada ya taji

http://www.dfb.de/fileadmin/Image_Archive/News/145498756-1_02_34170_p880722.jpg
NAHODHA wa timu ya taifa ya Ujerumani, Philipp Lahm ametangaza kustaafu kutoka soka la kimataifa ikiwa ni siku chache tangu alipoiongoza nchi yake kunyakua taji la nne la Kombe la Dunia katika Fainali zilizofanyika nchini Brazil.
Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na Shirikisho la Soka Ujerumani – DFB, beki huyo wa Bayern Munich mwenye umri wa miaka 30 amefanya uamuzi huo, baada ya kumpigia simu rais wa DFB Wolfgang Niersbach.
Niersbach alimshukuru kwa mchango wake wa miaka kumi katika timu ya Ujerumani ambapo pia aliibuka kuwa kielelezo kwa chipukizi wengine. Kushinda Kombe la Dunia ni kama kilele cha kazi yake ya kandanda kufikia sasa, ambayo inajumuisha pia taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, mataji sita ya Bundesliga na sita ya Kombe la Shirikisho la Soka Ujerumani.
Lahm alianza kazi yake ya kandanda mnamo Februari 2004 katika ushindi wao wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Croatia. Kisha akaichezea Ujerumani mechi 113 na kufunga magoli matano. Kabla ya kushinda Kombe la Dunia la 2014, Lahm na timu yake waliibuka washindi wa tatu Kombe la Dunia mwaka wa 2006 na 2010, na wakawa makamu bingwa wa dimba la Euro 2008. Pia alicheza katika Euro 2004 na 2012.
Mkataba wa Lahm na mabingwa wa Bundesliga Bayern ulirefushwa kabla ya Kombe la Dunia na utakamilika mwaka wa 2018.

No comments:

Post a Comment