STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, July 19, 2014

Kuziona Stars na Mambas ni Sh 7,000 tu

http://kandanda.galacha.com/wp-content/themes/LondonLive/thumb.php?src=http://kandanda.galacha.com/wp-content/uploads/2014/06/TAIFA1.jpg&w=467&h=278&zc=1&q=100
MASHABIKI wa soka watazishuhudia timu za taifa za Tanzania, Taifa Stars na Mambas ya Msumbiji kwa Kiingilio cha Sh. 7,000 tu katika pambano hilo litakalochezwa kwenye uwanja wa Taifa kesho kuwania nafasi ya kutinga kwenye makundi ya kwenda kwenye Fainali za Kombe la Afrika 2015 zitakazofanyika nchini Morocco.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Boniface Wambura, viingilio kwa mechi hiyo vitakuwa bni sh. 7,000 na sh. 30,000 kwa viti maalumu 4,500 tu.
Kuanzia asubuhi ya leo Jumamosi tiketi za kielektroniki zimeanza kuuzwa pia katika magari maalumu kwenye vituo vya Buguruni Shell, Dar Live Mbagala, Ferry Magogoni, Kigamboni, OilCom Chang’ombe, OilCom Ubungo, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa (Kariakoo), TCC Club Chang’ombe na Uwanja wa Taifa.

 Aidha tiketi zinapatikana kupitia M-PESA kwa kupiga *150*00# kisha bonyeza 4, bonyeza tena 4 kisha weka namba ya kampuni 173399 kisha ingiza 7000 kama namba ya kumbukumbu ya malipo, kisha andika tena 7000 kwenye weka kiasi, kasha weka namba ya siri na baadaye bonyeza  1 kukubali.

 Utapokea ujumbe wenye orodha ya vituo vya MaxMalipo vya kuchukua tiketi ukiwa na namba ya uhakiki wa malipo yako.

 Vituo vya MaxMalipo vya kuchukulia tiketi ni mgahawa wa Steers uliopo mtaa wa Samora/Ohio, maduka makubwa ya Uchumi Supermarket (Quality Centre, Tabata Segerea na kituo cha daladala Makumbusho), Sheer Illussions (Millennium Tower na Mlimani City), maduka makubwa ya TSN Supermarket (City Centre, Kibo Tegeta na Upanga).

 Vodashop (Ubungo na Mill Pamba), Shop Mwenge (Born to Shine), Puma Petrol Station (Mwenge na Uwanja wa Ndege), Engen Petrol Station (Mbezi Beach), Big Bon Petrol Station (Kariakoo, Sinza Mori, Mbagala na Temeke), YMCA (Posta Mpya), City Sports Lounge (Posta), Uwanja wa Taifa) na Uwanja wa Karume.

No comments:

Post a Comment