STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 24, 2014

Arsenal chupuchupu ugenini, Chelsea, Swansea zazidi kupeta

Diego Costa kazini

Arsenal wakishangilia mabao yao ya kusawazisha nyumbani kwa Everton
ARSENAL iliyokuwa ugenini ililazimika kusubiri mpaka dakika za jioni kuweza kuchimoa bao mbele ya Everton na kuambulia pointi moja katika mechi yao ya pili ya Ligi Kuu ya England.
Bao la dakika ya mwisho la Olivier Giroud liliiokoa Arsenal kulala ugenini kwa Everton na kutoka sare ya 2-2.
Vijana wa Arsene Wenger walitanguliwa kufungwa bao dakika ya 19 kupitia kwa Seamus Coleman kabla ya  Steven Naismith kuwaongezea wenyeji bao la pili dakika ya 45 lililoonekana dhahiri ni la kuotea.
Hata hivyoi katika kipindi cha pili baadaya mabadiliko kadhaa yaliisaidia Arsenal kurejea na nguvu mpya na kurejea bao moja baada ya jingine dakika 10 za mwisho.
Baoa la kwanza la Ze Gunners lilifunmgwa na Aaron Ramsey katika dakika ya 83  kabla ya Giroud kuipa timu yake pointi moja kwa kusawzaisha bao dakika ya 90.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo Chelsea waliendelea kukalia kiti cha uongozi baada ya mapema kupata ushindi wa mabao 2-0, huku West Ham ikizinduka ugenini na kupata ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya
Crystal Palace, huku Aston Villa ilibanwa nyumbani na Newcastle United kwa kutoka suluhu ya kutofungana.
Southampton iliendelea kuchechemea kwa kulazimishwa suluhu nyumbani na West Bromwich na Swansea inaendeleza ubabe baada ya wiki iliyopita kuitoa nishai Manchester United, iliifumua Banley kwa bao 1-0.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo mitatu, Hull City itakuwa nyumbani kupepetana na Stoke City, Tottenham Hotspur itaikaribisha QPR na Sunderland itaikaribisha Manchester United na kesho Manchester Citry itakuwa dimba la nyumbani kuumana na Liverpool.

No comments:

Post a Comment