STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 24, 2014

Neymar majanga Barcelona, La Liga yaanza kwa kishindo

http://taroudantnews.com/fichiersTrdnt/uploads/naymar1.jpgKLABU ya Barcelona imepata pigo kubwa kuelekea katika mchezo wao wa ufunguzi wa La Liga dhidi ya Elche utakaochezwa leo Jumapili kutokana na taarifa za kukosekana kwa Neymar katika mchezo huo wa Camp Nou kutokana na majeruhi.
Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil, ndio kwanza alikuwa ameruhusiwa kucheza na madaktari wa timu hiyo baada ya kupona majeruhi ya mgongo aliyopata katika Kombe la Dunia lakini sasa anakabiliwa na majeruhi mengine. 
Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo, imedai kuwa Neymar alikuwa akilalamika maumivu katika kifundo chake cha mguu wa kushoto na baada ya vipimo imegundulika kuwa ana matatizo ambayo yatachukua muda kidogo kupona. 
Taarifa hiyo imeendelea kudai kuwa kurejea mazoezini kwa mchezaji huyo kutategemea kumalizika kwa maumivu hayo hivyo ni wazi hatakuwepo katika mchezo wa leo. 
Neymar alicheza mechi 26 za La Liga msimu uliopita na kufunga mabao saba lakini msimu huu unaonekana tayari ameuanza vibaya kwa maumivu.
Kipute cha ligi hiyo ya Hispania kilianza usiku wa jana kwa kushuhudiwa Malaga wakitamba nyumbani kwa kuitandika Athletico Club bao 1-0, Sevilla ikilazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Valencia, huku Granada ikivuna ushindi nyumbani dhidi ya Deportivo la Coruna kwa kuilaza mabao 2-1 na Almeria na Espanyol wakitishana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

No comments:

Post a Comment