STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 24, 2014

Di Maria njia nyeupe kutua Manchester United

Angel di María na Sami Khedira ni wazi sasa wako mguu mmoja nje ya Real Madrid baada ya kutupwa nje ya Kikosi kilichoteuliwa kuivaa Atletico Madrid Ijumaa Usiku huko Estadio Vicente Calderon kwenye Mechi ya Marudiano ya Supercopa de Espana ambayo Real walichapwa 1-0.
Awali wote wawili walitajwa kwenye Kikosi cha Wachezaji 22 kwa ajili ya Mechi hiyo na Atletico Madrid kwa mujibu wa Jarida la Marca wakimnukuu Kocha wa Real Carlo Ancelotti.

Lakini walipofika huko Valdebebas, Kituo cha Mazoezi cha Real, Di Maria na Khedira walijulishwa kuwa hawamo kwenye Kikosi cha kwenda kwenye Mechi na Atletico na hilo liliwakera sana Wachezaji hao kwa mujibu wa Marca.
Wakati Di Maria akiamua kurudi Nyumbani kwake, Khedira aliamua, bila ya ruhusa ya kusafiri ya Real, kupanda Ndege kwenda kwao Germany, Mji wa Leipzig kumshuhudia Ndugu yake akicheza Mechi.

Hadi sasa haijajulikana wazi Wachezaji hao wanakwenda wapi mbali ya Kocha Ancelotti kutoboa kuwa wote wamekataa Mikataba mipya na Di Maria ameomba kuhama.
Hadi sasa Di Maria anahusishwa sana na kuhamia Manchester United na Leo zimeibuka ripoti kuwa Khedira yeye atakwenda Bayern Munich kuchukua nafasi ya Majeruhi wa muda mrefu Javi Martinez.Jarida la Marca, ambalo lipo karibu mno na Klabu ya Real Madrid, limethibitisha Wachezaji hao wawili watahama rasmi Wiki ijayo.
Rojo tayari alishajiunga na Man United.

No comments:

Post a Comment