STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 24, 2014

WAZIRI Wassira awafunda wajasiriamali

http://ippmedia.com/media/picture/large/wasira%20ipp(1).jpg
NA SULEIMAN MSUYA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Sera na Mipango Stephen Wassira amesema wakati umefika kwa Watanzania kuondokana na mfumo wa kuuza malighafi katika masoko ya ndani na nje ya nchi ili waweze kupata faida kubwa ya mazao wanayozalisha.
Wassira alisema hayo wakati alipohudhuria Mkutano wa Bodi ya Magavana ya Proffensial Trade Association (PTA) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Alisema kwa miaka mingi wakulima wa Tanzania wamekuwa wakiuza malighafi badala ya bidhaa iliyokamilika kutokana na malighafi hiyo halia ambayo inachangia wanyonywe na wanunuzi.
Waziri huyo wa Nchi Ofisi ya Rais Sera na Mipango alisema ili kuhakikisha kuwa wakulima wanapata mabadiliko kutokana na kilimo Serikali inaendelea kufanya juhudi za kuhakikisha kuwa viwanda vinakuwepo katika maeneo ya wakulima walipo.
“Kilimo ni moja ya sekta nzuri sana ila huwezi kuona manufaa yake iwapo wewe kila siku unauza malighafi kwa wenzako waliondelea jambo ambalo wanahakikisha kuwa linakwisha”’ alisema.
Wassira alisema Serikali inaendelea kutafuta wawekezaji ambao watakuja kuwekeza na  kuwa kichochoe cha kukuza uchumi wa wakulima na jamii kwa ujumla.
Aidha alizungumzia mafanikio yaliyopatikana kupitia Benki ya PTA kwa Tanzania ambapo alisema kuwa imetoa msaada wa uboreshaji wa bandari ya Dar es Salaam, Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julias Nyerere.
Waziri Wassira  alisema serikali itaendelea kushirikiana na benki hiyo ya maendeleo ya PTA ili kuhakikisha kuwa inaendeleza sekta mbalimbali hasa kupitia mpango wa pili wa maendeleo ambao unatarajiwa kuaanza hivi karibuni.
Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda alisema juhudi zao ni kuhakikisha kuwa  PTA inakuwa na ofisi zake hapa nchini ili kuhakikisha kuwa wanashiriki moja kwa moja kusaidia kutatua changamoto zilizopo hapa nchini.
Alitoa wito kwa PTA kusaidia Tanzania katika sekta ya miundombinu, kilimo, ujasiriamali na umeme akiamini kuwa maeneo hayo yakipata ufumbuzi ni wazi kuwa uchumi wanchi utakuwa kwa kasi.
Pinda alisema PTA ni moja ya  mabenki ambayo hayana riba kubwa kwa mikopo yake inayotoa hivyo Tanzania itaendelea kushirikiana nayo ili kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii yake.
Waziri Mkuu alisema ni vyema wawekezaji wa ndani kutumia benki hiyo katika kuomba mikopo ambayo ina riba ndogo ili waweze kuwekeza ndani ya nchi yao.
Alisema kupitia benki hiyo ni wazi wajariamali wadogo na wakati watafaidika jambo ambalo litachochea ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment