STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 24, 2014

Mshale wa Aisha Bui kutupwa wiki ijayo siyo kesho tena

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiXMubpSkoyEQuwMbeI-V_WEnpb2FZ55PnmSTksu9SQcbRJoiwNFcLnFxjnDHjjzi94I0uF5_h6NYkWE5ZClymhKjniWp9O0pMjTGLQRCQHBZRPqT21Lfx13uwenFVycRWQjPOaQzcETW0/s1600/DUI.jpg
Aisha Bui
FILAMU mpya ya muigizaji nyota wa filamu nchini, Aisha Fat'hi 'Aisha Bui' iitwayo 'Mshale wa Kifo' inatarajiwa kuingia sokoni wiki ijayo baada ya mipango ya kuitoa leo Jumatatu kushindikana.
Aidha mwanadada  ametamba kuwa filamu hiyo ni mwanzo wa uhondo ambao kampuni yake ya Bad Girl Film's imepanga kuwapa mashabiki wa filamu Tanzania.
Akizungumza na MICHARAZO, Aisha Bui alisema filamu hiyo aliyoigiza na wakali kama Mzee Chilo, Gabo wa Zagamba na wengine ilikuwa itolewe leo, lakini kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake itaingia sokoni Septemba 4, huku ikijipanga kuandaa kazi nyingine kali zaidi na hiyo.
Aisha Bui, alisema japo filamu hiyo ni kazi yake ya kwanza kuiandaa, lakini kwa jinsi ilivyoandaliwa kwa umakini mkubwa ni wazi mashabiki watajua ujio wake mpya siyo wa kubahatisha.
"Naiachia filamu yangu mapema mwezi ujao badala ya Jumatatu (leo), nawaomba mashabiki waniunge mkono kwa kununua nakala halisi, ili kuiwezesha kampuni ya Bad Girl kuendelea kuwapa uhondo zaidi, kuna makubwa yapo njiani kutoka kwangu," alitamba Aisha Bui.
Nyota huyo aliyecheza filamu mbalimbali ikiwamo ya Saturday Morning, Better Days, Not Without My Son, Continous Love, Revenge of Love, Mirathi, Pain of Love, Crazy Love na The Second Wife, alisema ndani ya filamu hiyo mpya inasimulia kisa cha mfanyabiashara wa dawa za kulevya ambaye anamlazimisha askari Polisi kumsaidia kupitisha mzigo wake.
Hata hivyo kazi haiwi rahisi na kuibua kashkash kwa binti wa askari huyo Myrine nafasi iliyochezwa na Aisha kufanywa kama chambo.
"Ni simulizi linalosisimua na kutia simanzi na bahati nzuri walioiigiza kuanzia mimi mwenyewe, Gabo, Mzee Chilo na wengine tumeitendea haki," alisema Aisha.

No comments:

Post a Comment