STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 24, 2014

Nani kutwaa taji la KAGAME Leo?!

http://www.umuseke.rw/wp-content/uploads/2013/08/APR-FC.jpg
APR
http://africanfootball.com/bp_images/Al_Merreikh_Team_1.jpg
El Merreikh
BINGWA mpya wa michuano ya Kombe la Kagame 2014 anatarajiwa kujulikana leo wakati wenyeji APR ya Rwanda na El Merreikh ya Sudan zitakapopepetana kwenye mchezo wa fainali kwenye uwanja wa wa Amahoro, Kigali.
Taji la michuano hiyo kwa sasa lipo wazi baada ya waliokuwa watetezi, Vital'O ya Burundi kung'oka mapema kwenye michuano hiyo ambayo ilishuhudia wawakilishi wa Tanzania, Azma wakitolewa kwa mikwaju ya penati katika hatua ya Robo Fainali.
Timu hizo mbili zilifuzu hatua hiyo baada ya kushinda mechi zao za Nusu Fainali kwa mikwaju ya penati, APR wakiwatoa maafande na ndugu zao POlisi kwa mikwaju 4-3 baada ya kumaliza dakika 120 bila kufungana wakati Wasudan waliitoa KCCA ya Uganda kwa penalti 3-0 baada ya kumaliza dakika 120 wakitoka sare ya mabao 2-2.
Mechi hii ya leo inatarajia kuwa na upinzani mkubwa kutokana na ubora wa vikosi vya timu zote ambazo zinaundwa na vijana wadogo wenye vipaji, hali ambayo inakubwa ngumu kujua kama ni E;l Mereikha watakaotwaa taji lao la tatu la michuano hiyo au APR.Kabla ya mechi hiyo kutatanguliwa na mechi ya mshindi wa tatu kati  ya Polisi na KCCA.

No comments:

Post a Comment