STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 22, 2014

Babu Tale acharuka tuhuma za Diamond na Dawa za Kulevya

Diamond (kulia) akiwa na Meneja wake, Babu Tale na Aunty Ezekiel
BAADA ya chombo kimoja cha habari kuandika habari juu ya tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya kwa nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul 'Diamond', Meneja wake Khamis Tale 'babu Tale' ameamua kufunguka na kuwachana walioandika habari hiyo kama anavyosomeka hapo chini;
"Tunalipwa milioni 20 show moja, tunalipwa dola elfu 25,000 show moja, hii ni zaidi ya madawa ya kulevya. “We get more money from music, sio kwenye madawa ya kulevya, hatufanyi hizo biashara na kama wanahisi sisi tunafanya tunawaruhusu watufanyie investigation hata kwa muda wa miaka kumi ina maana tunavyopita pale airport hawana vifaa vya kutuchunguza? Ipo wazi hata Global walishindwa kufanya kazi na sisi kwa sababu sisi ni wakubwa.
Sasa leo hii tunauza madawa ya kulevya kwa sababu tunakomaa kwenye bei zetu. “September tunafanya show kubwa ya Unplugged na msanii wa kwanza hapa kufanya ile show ni Diamond na ile show hawalipi hela ya kis**e.
Wataendelea kuona watu wanauza madawa ya kulevya, hakuna msanii wa Tanzania anayefanya show kwa walau dola elfu 10,000 ni Diamond peke yake wengine ni dola 2000, 2500 elfu 3,000 mwisho.
Tuna show Marekani show kumi na tano (15), show kumi na tano dola elfu ngapi? Na kwa hapa Tanzania hatufanyi show chini ya dola elfu 15,000.”

No comments:

Post a Comment