STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 22, 2014

Extra Bongo, Omar Tego kuwasindikiza Masai Safari Band

BENDI ya Extra Bongo 'Wazee wa Kizigo' wanatarajiwa kusindikiza uzinduzi wa albamu ya kwanza ya bendi ya Masai Safari utakaofanyika Agosti 30.
Uzinduzi wa albamu hiyo iitwayo 'Hakuna Kama Baba' utafanyika kwenye ukumbi wa Lunch Time na kwa mujibu wa Rais wa Masai Safari, Francis Mwaisela, Extra Bongo ni kati ya watakaowasindikiza siku hiyo.
Mwaisela alisema makundi mengine yatakayokuwapo ukumbini kuwapia tafu siku hiyo ni Coast Modern linaloongozwa na waimbaji ndugu, Omar na Maua Tego.
"Extra Bongo, Omar Tego na dada yake Maua Tego na wasanii wengine wa muziki wa kizazi kipya ndiyo watakaotusindikiza siku ya uzinduzi wa albamu yetu utakaofanyika Agosti 30," alisema Mwaisela.
Rais huyo wa Masai Band alizitaja nyimbo zilizopo katika albamu hiyo ni 'Hakuna Kama Baba', 'NJia Panda', 'Mikoni ni Kazi', 'Ndoa ni Mipango ya Mungu', 'Usiwasikilize Wambea,' na Kilio Changu'.
"Kwa sasa tupo kenye mazoezi makali kwa ajili ya uzinduzi huo ambao tumepania kuweka rekodi nchini," alisema Mwaisela

No comments:

Post a Comment