STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 22, 2014

Di Maria aomba kuondoka Real Madrid

http://talksport.com/sites/default/files/styles/large/public/field/image/201308/angel_di_maria.jpg?itok=gPwE_rnHCARLO Ancelotti amebainisha kwamba Angel Di Maria anataka kuondoka Real Madrid na kwamba wanaangalia mpango wa kulimaliza suala lake kabla dirisha la usajili halijafungwa.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina amepoteza namba katika kikosi cha kwanza Madrid kufuatia kutua kwa James Rodriguez na Toni Kroos katika kipindi hiki cha usajili na amedhamiria kutafuta namba kwingineko.
Di Maria amekuwa akihusishwa sana na PSG na Manchester United katika miezi kadhaa iliyopita, lakini mabingwa hao wa Ligue 1 walisema hivi karibuni kuwa hawana mpango wa kumsajili winga huyo kutokana na sababu za kiuchumi, na hivyo kuiachia Man U nafasi kubwa ya kumpata.
"Ameniomba kuondoka katika kipindi hiki cha usajili. Amekataa ofa ya klabu ya kubaki Madrid, hivyo tunatafuta suluhisho," Ancelotti alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari.
"Tutapata suluhisho kwa Di Maria kabla ya dirisha kufungwa, lakini kwa sasa anabaki kuwa mchezaji wa Madrid. tuko katika hali ambayo mchezaji anatakiwa kujitafutia klabu mwenyewe.
"Kama Di Maria atashindwa kupata suluhisho mwenyewe, atabaki hapa. Tunamkaribisha na anaweza kuendelea kufanya kazi hapa. hakuna shida."
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26, aliyejiunga na Madrid akitokea Benfica katika kipindi hiki cha uhamisho cha 2010, ana mkataba na Madrid hadi 2018, lakini anaweza kuuzwa kwa euro milioni 60.

No comments:

Post a Comment