STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 22, 2014

Majanga yaanza mapema Arsenal, Arteta kuikosa Everton kesho

http://worldsoccertalk.com/wp-content/uploads/2013/08/mikel-arteta.jpg
MAJANGA yamezidi kuiandama Arsenal baada ya kiungo mkabaji wao, Mikel Arteta naye kuelekea chumba cha majeruhi kwa mechi mbili baada ya Jumanne kuumia kifundo cha mguu 'ankle' kwenye mechi ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Besiktas ya Uturuki.
Nahodha huyo wa Arsenal alitolewa nje katika dakika ya 50 kwenye Uwanja wa Olympic Ataturk baada ya kuumia wakati akiwania mpira dhidi ya mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Demba Ba.
Arsenal pia itamkosa Aaron Ramsey baada ya kutolewa nje kwa kadi mbili za njano katika kipindi cha pili kwenye mechi hiyo ya Uefa.
Arteta sasa ataikosa mechi ya Ligi Kuu England Jumamosi ugenini dhidi ya Everton pamoja na ile ya marudiano ya kuwania kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya  dhidi ya Besiktas itakayopigwa Jumatano kwenye Uwanja wa Emirates.
Jana alitarajiwa kufanyiwa uchunguzi zaidi lakini ni wazi kabla ya hapo alishaelezwa kuzikosa mechi mbili zijazo.
Chumba cha majeruhi cha Arsenal tayari kimeanza kupokea wagonjwa baada ya Yaya Sanogo na Kieran Gibbs kuwa majeruhi na kuikosa mechi dhidi ya Besiktas ambayo walitoka sare tasa huko Istanbul.
Haitakuwa rahisi kwa Arsenal katika mechi hiyo ya marudiano dhidi ya Besiktas, na zaidi kutokana na kuwakosa Aaron Ramsey na Mikel Arteta, lakini haijawahi kutolewa katika mechi hizo za mchujo za Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Hata hivyo, Mesut Ozil, Per Mertesacker na Lukas Poldolski watakuwamo kwenye kikosi cha Arsenal jambo ambalo linamshawishi kiungo Jack Wilshere kwamba wataonesha tofauti kubwa.

No comments:

Post a Comment