STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 22, 2014

Queen Darlin ageukia filamu, kuuza sura kwa ChekibudiDADA wa nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Diamond Platnumz, Mwajuma Abdul 'Queen Darling' anatarajiwa kuibuka kwenye anga za uigizaji baada ya kushirikishwa katika filamu iitwayo 'Kisebusebu'.
Filamu hiyo na muigizaji nyota nchini Nurdin Mohammed maarufu kama 'Chekibudi' imekamilishwa kurekodiwa hivi karibuni na inafanyiwa mchakato wa kuachiwa mwezi ujao.
Chekibudi aliiambia MICHARAZO kuwa, Queen Darling anayetamba na nyimbo kama 'Wajua Nakupenda', 'Maneno' na 'Wanatetemeka' pamoja na remix ya 'Nakomaa na Jiji', ameitendea haki filamu hiyo.
"Huwezi kuamini kama Queen Darling ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kwa jinsi alivyotenda haki mbele ya kamera," alisema Chekibudi na kuongeza mbali na msanii huyio filamu hiyo pia ameiigiza yeye (Chekibudi), Tiko Hassan na wakali wengine.
Wasanii kadhaa wa bongofleva wamekuwa pia wakitamba katika Bongo Movie kama Snura, Shilole a.k.a Shishi Baby na Hemed Suleiman a.k.a PHD.

No comments:

Post a Comment