KLABU ya AS Vita ya
DR Congo imeanza vema mbio zake za kucheza Fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuinyuka CS Sfaxien
ya Tunisia mabao 2-1.
Mabao ya Vita katika mchezo huo uliochezwa
katika Uwanja wa Tata Raphael jijini Kinshasa yalitupiwa kimiani na
Firmin Ndombe Mubele na Heritier Luvumbu Nzinga huku lile la kufutia
machozi la Sfaxien likifungwa na Ali Maaloul.
Ushindi huo unaiweka katika nafasi nzuri Wakongo hao kwa mechi ya marudiano itakayofanyika wikiendi hii mjini Tunis.
Vita watakwenda katika
mchezo wao wa marudiano wakihitaji sare ya aina yoyote inaweza
kuwapeleka fainali ambapo watakutakana na aidha ES Setif ya Algeria
au TP Mazembe ya DRC.
Sfaxien ambao ni mabingwa wa Kombe la Shirikisho
na Super Cup walionekana kuzimiliki vyema dakika 20 za mwisho katika
mchezo huo lakini walishindwa kutafuta nafasi ya kusawazisha.
Katika mchezo wa kwanza 'ndugu' zao TP Mazembe walichapwa mabao 2-1 na wapinzani wao ambao watarudiana nao wikiendi hii mjini Lubumbashi na kama timu hizo za Kongo zitafuzu fainali itakayopigwa Octoba 25-26 na Novemba 1-2 itakuwa ni mara ya kwanza kwa timu Chini ya Jangwa la Sahara kukutana pamoja katika hatua hiyo.
No comments:
Post a Comment