STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, September 23, 2014

Bilioni 20 zahitajika kutatua tatizo la Ajiora nchini

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj-F5hwnHLukOOHecjhZ-ghBDejeN6VOEVNIpFPCcLyvhzRQSnpxPJQMoPK0TMjEI6_GHXln6t7ZsHQv5IPO-4lzTHCdxZsY5zg0yjg0u1lXUwCocg-aXzVOF9kMVqArWiwC4b0HCaqkiE/s1600/2.JPG
Dk Kisui (kushoto) akifafanua jambo
Na Kipimo Abdallah
WIZARA ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imesema inahitaji shilingi bilioni 20 kila mwaka ili iweze kupunguza tatizo la ajira hapa nchini.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Uwezeshaji na Uhamasishaji wa Wizara hiyo Dk. Steven Kisui  wakati akijibu swali la mwandishi wa habari hii.
Alisema bajeti wanayotengewa haitoshelezi mahitaji ya vijana jambo ambalo linachelewesha juhudi za kupunguza ukubwa wa tatizo hilo ambalo linatajwa kama janga la Taifa.
Dk. Kisui alisema mahitaji ni makubwa kutoka kwa vijana mbalimbali nchini ambao wamejiunga katika SACCOS ila uwezo wa Serikali ni mdogo hivyo zoezi hilo
linachukua muda kutatuliwa.
"Kusema ukweli bajeti ya shilingi bilioni 6 hatuwezi kufikia malengo lakini tutaenda hivyo hivyo hadi tufikie muafaka,kwani kiukweli ni ndogo mnno", alisema.
Kisui alisema juhudi za Wizara ni kuhakikisha kuwa hicho kidogo kinachopatikana kinawafia walengwa ambao watakuwa wamefikia vigezo pamoja na ukweli kuwa bilioni 20 zingeweza kutatua tatizo.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Concilia Nyibitanga alisema hadi kufikia sasa ni Halimashauri 42 kati ya 169 ambazo vijana wake ndio wametengeneza vikundi vya SACCOS.
Alisema mwamko wa Halimashauri kuhakikisha kuwa vikundi vinakuwepo imekuwa mdogo sana jambo ambalo linakwamisha juhudi za Serikali.
"Pamoja na juhudi za serikali katika kuhakikisha kuwa vijana wanafikiwa bado mwamko ni mdogo sana katika Halimashauri nyingi jambo ambalo linaweza kuwa kikwazo", alisema.
Nyibitanga alisema fedha hizo ambazo zinakopeshwa kwa riba ndogo lengo lake ni kuhakikisha kuwa vijana wanajiajiri ili kuhakikisha kuwa wanakabilianana changamoto zinazowakabili.

No comments:

Post a Comment