Na Kipimo Abdallah
MFUKO wa Pensheni wa PSPF umetoa shilingi milioni 10 kwa ajili ya kudhamini siku ya Msaani Tanzania.
Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Abdul Njaidi wakati akizungmza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Alisema lengo la PSPF kujitolea kudhamini siku hiyo na katika kuangalia sekta nzima ya sanaa kwa kuwawezesha, kuwapa mafunzo wasanii ili waweze kujikwamua kiuchumi hapa nchini.
Njaidi alisema PSPF imekuwa ikijikita katika kuwapatia mafao watumishi wa sekta mbalimbali zilizo rasmi kwa miaka mingi ila kwa kipindi cha hivi karibuni hata sekta isiyo rasmi inahusishwa wakiwepo wasanii.
"Kwa kuanza sisi PSPF tumeamua kudhamini siku ya Msanii Tanzania kwa kutoa milioni 10 ambapo tunaamini zitasaidia mchakato huo", alisema.
Aidha Njaidi alisema pamoja na kudhamini siku hiyo PSPF inaendelea na kupokea wanachama kutoka sekta mbalimbali ambao wapo tayari kwa malengo yao baadae.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Haak Neel Production Company Limited Geofrey Katulo alisema siku ya Msanii ni mradi uliobuniwa na Baraza la SanaaTaifa (BASATA) na utaendeshwa kwa ubiia wa Haak Neel Production Company Limited.
Alisema mradi huo ulibuniwa ili kuungana na wenzao duniani kuadhimisha siku siku ya kimataifa ya Msanii ambayo huadhimishwa kila ifikapo Oktoba 25 kwa lengo la kumtambua msaani, kazi zake pamoja na mchango wake katika jamii.
Katula alisema kauli mbiu ya siku ya msaanii mwaka 2014 ni "Sanaa ni Kazi" ambapo fani zitakazohusika katika maadhimisho hayo ni taarabu, muziki wa dansi, ngoma za asili, muziki wa msanii kutoka nje ya nchi.
Fani zingine ni uchezaji shoo, dansi za mitaani, bongo fleva, maonyesho ya mitindo ya mavazi, sanaa kwa watoto na maonyesho ya sanaa za ufundi pamoja na semina.
No comments:
Post a Comment