IMEBAINIKA wazi kuwa ni ndoto kwa Fainali za Soka za Kombe la Dunia za mwaka 2022 kufanyika Qatar.
Mjumbe wa kamati ya
utendaji ya Shirikisho la Soka Duniani,FIFA, Theo Zwanziger amefichua kuwa ni vigumu fainali hizo kuchezwa nchini humo kutokana
na hali ya joto kali katika nchi hiyo.
Zwanziger ambaye ni
raia wa Ujerumani aliliambia jarida la michezo la Bild jana kuwa
anadhani mwisho wa siku michuano ya Kombe la Dunia 2022 haitafanyika
katika nchi hiyo.
Mjumbe huypo aliendelea kudai kuwa watabibu wamesema
hawatakubalia kuwajibika kama michuano hiyo itafanyika katika hali ya
hatari kama hiyo.
Japo Qatar wamesisitiza ambao ni matajiri wakubwa wa
mafuta wamesisitiza kuwa wanaweza kuandaa michuano hiyo majira ya
kiangazi kwa kutumia teknolojia ya vipoza hewa katika viwanja vyake,
sehemu za mazoezi na mahali watakapofikia mashabiki bado kumekuwa na
wasiwasi mkubwa kuhusiana na afya za wachezaji na mashabiki watakaokuja
kushuhudia michuano hiyo.
Zwanziger amesema anajua wanaweza kuweka
vipoza hewa viwanjani lakini Kombe la Dunia halichezwi viwanjani pekee
kwani mashabiki kutoka duniani kote watakwenda na kusafiri katika hali
hiyo ya joto jambo ambalo ni hatari kwa afya na maisha yao. Michuano ya
mwaka 2022 imekuwa ikileta mjadala mkubwa huku rais wa FIFA Sepp Blatter
akikiri kuwa walifanya makosa kuipa Qatar kuandaa michuano hiyo na
kutaka kuangalia uwezekano wa kuamisha michuano hiyo ichezwe katika
majira ya baridi.
No comments:
Post a Comment