BAADA ya Mario Balotelli kushindwa kuvaa vyema viatu vya Luis Suarez, klabu ya Liverpool imesema inajiandaana kutenga pauni milioni 30 kwa ajili ya kumnasa wa PSG, Ezequiel Lavezzi katika usajili wa mwezi Januari.
Vijogoo hao wa Anfield wamekuwa wakidaiwa kumnyemelea Strika huyo katika sehemu kubwa ya
kipindi cha uhamisho wa wachezaji cha kiangazi lakini mpango huo
ulikwama.
Hata
hivyo kwa mujibu duru za soka nchini humo zimedai kuwa, meneja Brendan Rodgers
anajipanga kujaribu tena mpango huo kwa mabingwa wa soka wa nchini
Ufaransa wakati dirisha la usajili litakapo funguliwa tena mapema
mwakani.
Liverpool
imekuwa ikihaha kusaka mshambuliaji tangu mapema kutokana na pengo lililoachwa na Suarez aliyeuzwa Barcelona na pia kuumia kwa Daniel Sturridge.
Ilimsajili Mario Balotelli kwa Pauni Milioni 16, lakini mpaka sasa dau hilo halijaleta matunda kutokana na Muitalia huyo mwenye asili ya Ghana kushindwa kufunga mabao na huku akiwa mwingi wa vituko.
Liverpool
iko katika nafasi ya sita katika ligi ikiwa nyuma ya vinara wa ligi
hiyo Chelsea kwa alama tisa baada ya michezo minane kukamilika.
Lakini
Rodgers bado ana matumaini ya kuimarihsa kikosi chake mwezi Januari ili
kuweza kupata nafasi nyingine ya kushiriki ligi ya mabingwa Ulaya msimu
mwingine.
Kikosi hicho jana kilikumbana na kipigo cha aibu toka kwa Real Madrid baada ya kufungwa 3-0 ikiwa ni marfa ya kwanza tangu mwaka 2009 ambapo timu hiyo ilikuwa ikiwatambia Mabingwa hao wa Ulaya.
No comments:
Post a Comment