Ronaldo akifunga bao la kwanza la Real Madrid |
Benzema akishangilia moja ya mabao yake jana |
Balotelli akiwa na Pepe |
Pongezi zako kaka! |
Najar akiwatungua Arsenal |
Ronaldo alifunga bao la kuongoza dakika ya 23 likiwa ni bao la 69 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kutokana na mechi 105 na kuwa sawa na Messi aliyecheza mechi 88 tu na kusaliwa mabao mawili kumfikia Raul.
Katika pambano hilo lililoshuhudiwa mshambuliaji wa kiitalia, Mario Balotelli akitolewa wkaati wa mapumziko na kubadilishana jezi na beki Pepe Karim Benzema alifunga mabao mawili.
Benzema anayesifiwa na Ronaldo kuwa ndiye namba 9 bora duniani alifunga dakika ya 30 na 41 na kuwazamisha vijana wa Brendan Rodgers aliyenukuliwa hatamvumilia tena Balotelli kwa alichokifanya uwanjani jana.
Katika mechi nyingine ya kundi hilo la B, Ludogorets Razgrad imeichapa bao 1-0 Basel, huku katika mechi nyingine Arsenal ilitakata ugenini baada ya kuilaza Anderlecht mabao 2-1.
Mabao ya 'usiku' ya Kieran Gibbs na mtokea benchi, Lukas Podolski yaliiokoa Arssenal isizame Brussels, Ubelgiji.
Wenyeji walipata bao dakika ya 72 kupitia Andy Najar kabla ya Gibbs kufunga dakika 88 na Podolski asiye na furaha Emirates kwa sasa kufunga dakika za nyongeza.
Arsene Wenger amedokeza kuwa hawana mpango wa kumuuza Mjerumani huyo mwenye asili ya Poland japo mwenyewe amekuwa akisisitiza kuwa Januari ataondoka Emirates akatafute mahali atakapoaminiwa na kucheza kwa raha zake.
No comments:
Post a Comment