Pambano lililoibeba Tanzania katika orodha mpya ya FIFA |
Kwa mujibu wa orodha mpya Tanzania iliyokuwa ya 115 katika orodha ya mwezi Septemba, imepanda hadi nafasi ya 110 hii ni kutokana na ushindi wake wa mabao 4-1 dhidi ya Benin.
Hata hivyo ni kwamba Uganda imeendelea kuwa juu ya nchi zote wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), pamoja na kushuka kwa nafasi tano hadi ya 84.
Algeria ndiyo kinara wa nchi za Afrika ikikamata nafasi ya 15 duniani, wakati Mabingwa wa Dunia Ujerumani imeendelea kushika nafasi ya kwanza duniani ikiziongoza Argentina na Colombia wanaoifuata.
Orodha hiyo inaoonyesha Ubelgiji, Uholanzi, Brazil, Ufaransa, Uruguay, Ureno na Hispania ndizo zinazofunga 10 Bora, ilihali Ivory Coast waliokuwa wakiiongoza kwa muda mrefu Afrika ikiporomoka hadi nafasi ya 25 Duniani.
Ghana imeshuka kwa nafasi mbili hadi ya 35, wakati Misri imepanda kwa nafasi 23 hadi ya 38 na Cameroon imepanda kwa nafasi mbili hadi ya 40, ikifuatiwa na Senegal na Nigeria ambazo zote zimeporomoka kwa nafasi tano.
Benin iliyopigwa 4-1 nq Tanzania yenyewe imeporomoka toka nafasi ya 78 hadi 86.
ANGALIA 30 BORA DUNIANI: 1 Germany
2 Argentina
3 Colombia
4 Belgium
5 Netherlands
6 Brazil
7 France
8 Uruguay
9 Portugal
10 Spain
11 Italy
12 Switzerland
13 Chile
14 Croatia
15 Algeria
16 Costa Rica
17 Mexico
18 Greece
19 Ukraine
20 England
21 Romania
22 Czech Republic
23 USA
24 Slovakia
25 Côte d'Ivoire
26 Bosnia and Herzegovina
27 Ecuador
28 Iceland
29 Austria
30 Russia
No comments:
Post a Comment