STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, March 7, 2015

Azam yalipa kisasi JKT , Coastal yabanwa Tanga

Mfungaji wa bao pekee la Azam

BAO pekee kutoka kwa Mrundi, Didier Kavumbagu limeiwezesha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara kulipa kisasi kwa JKT Ruvu.
Azam walipata ushindi huo kwenye uwanja wa Chamazi na kuifanya timu hiyo kuzidi kuwapumulia Yanga waliopo kileleni ambao kesho watashuka dimbani kuvaana na Simba.
Kavumbagu alifunga bao hilo lililokuwa la tisa kwake msimu huu katika ligi hiyo katika dakika ya 17 akiunganisha mpira wa krosi ya beki Shomari Kapombe na yeye kuufungwa kwa kichwa.
Azam imefikisha pointi 30, moja pungufu na ilizonazo Yanga yenye 31 ambao kesho watakuwa vitani dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Taifa/ Kati mechi ya mkondo wa kwanza JKT Ruvu ndiyo iliyokuwa timu ya kwanzsa iliyovunja rekodi ya Azam ya kushinda mechi mfululizo 38 baada ya kuichapa bao 1-0.
Katika mchezo mwingine uliochezwa leo mabingwa wa zamani wa soka nchini, Coastal Union kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Mkwakwani Tanga walilazimishwa sare ya mabao 2-2 na Kagera Sugar.
Mabao ya Coastal yalifungwa na Seleman Kibuta na Rama Salim wakati wageni walipata mabao yake kupitia kwa Atupele Green na Enock Kyaruzi.
Pambano jingine kati ya Polisi Moro dhidi ya Ruvu Shooting limeshindwa kufanyika mpaka siku ya Jumanne kutokana nna uwanja wa Jamhuri Morogoro kutumika na shughuli za sherehe za Siku ya Wanawake inayofikia kilele kesho Jumapili.

No comments:

Post a Comment