STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, May 22, 2016

Wazee Yanga wamng'ang'ania Manji Jangwani

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji
HAKUNA namna. Baraza la Wazee wa Yanga wameibuka na kuweka wazi kuwa, wanamuunga mkono Mwenyekiti wao aliyemaliza muda wake, Yusuf Manji, kuelekea kenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Juni 25 mwaka huu.
Manjia amekaa madarakani kwa miaka miwili nje ya utaratibu wa Katiba ya klabu hiyo ya Jangwani.
Akizungumza na Wanahabari leo Jumapili jijini Dar es Salaam, akiweka bayana msimamo wa Wazee wa Yanga akiwa kwa pamoja na Mwenyeviti wa matawi wa mkoa wa Dar es salaam,  Katibu wa Baraza hilo Ibrahim Akilimali, alisema kuwa, wanamuunga mkono Manji kwa asilimia zote kwani ameweza kuisaidia timu hiyo toka akiwa mdhamini mpaka kufikia kuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo.
"Kwa upande wa Baraza la Wazee tunamuunga mkono Manji kwani toka Yanga imekuwa chini yake kumekuwa na mafanikio makubwa sana ikiwemo kuweza kuingia hatua ya makundi Kombe la Shirikisho na kama kuna masuala mengine ikiwemo ya uwanja uongozi mpya utakapoingia tutakaa nao kuweza kujua tunafikia wapi malengo yetu ya kujenga kwani tumeshafikia kwenye hatua bado kibali tu," alisema Akilimali.
Akilimali alisema, watu wasitake kuangalia suala la Uwanja kwa Manji tu, bali wakumbuke kuwa kuna viongozi wengine wamepita na hawajajenga cha msingi ni kuangalia wapi tunaelekea na nini kinachotakiwa kufanyika kwa maendeleo ya klabu yao.

Wazee hao walisema kwa pamoja kuwa mbali na hilo pia wanawapongeza wachezaji na benchi la ufundi kwa hatua nzuri waliyofikia ya kuchukua ubingwa kwa mara ya 26 pamoja na kuingia kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirishiko ikiwa ni moja mafanikio wanayojivunia chini ya Manji.

No comments:

Post a Comment