STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, February 12, 2013

Shaa wa Wakilisha achia mpya akiapa raha kwa mashabiki


Msanii Shaa katika pozi

MWANADADA mkali wa muziki wa kizazi kipya, Sarah Kais 'Shaa', aliyekuwa kimya kwa kitambo, ameibuka na 'ngoma' mpya iitwayo 'Promise', akiapa kuwapa raha zaidi mashabiki wake.
Shaa, mkali aliyeibuliwa na shindano la Coca Cola Pop Star na kuja kuunda kundi la pamoja na wakali wenzake wawili, Langa na Witness lililoitwa 'Wakilisha', alisema wimbo huo mpya ni salamu kwa mashabiki wake 2013.
Msanii huyo alisema baada ya kimya tangu aachie wimbo wake uitwao 'Siri ya Penzi', amefyatua ngoma hiyo mpya akiwa mbioni kuendelea kufyatua moja moja ili kuwapa raha mashabiki wake.
"Hizi ni salamu zangu za 2013, nimeachia 'Promise' na kwa sasa najipanga kwa ajili ya vitu vingine vikali ili kuonyesha kuwa 'Shaa' bado nipo na ukali wangu ni ule ule," alisema Shaa.
Msanii huyo alisema kwa sasa anafanya kazi chini ya usimamizi wa Babu Tale na umeneja wa Master J na kwamba mashabiki wake waliomiss kitambo watarajie makubwa zaidi kuliko ilivyokuwa siku za nyuma.

No comments:

Post a Comment