STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, February 12, 2013

Uchaguzi wa FRAT upo palepale Siku ya Wapendanao

Na Boniface Wambura
UCHAGUZI Mkuu wa viongozi wa Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) unafanyika Februari 14 mwaka huu mjini Morogoro kama ulivyopangwa, tofauti na taarifa wanazopewa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho.

Kwa mujibu wa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya FRAT, Damas Ndumbaro, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa FRAT wanatakiwa kufika Morogoro keshokutwa (Februari 12 mwaka huu) . Pia wapiga kura na wagombea wanatakiwa kulipia ada za uanachama kwa mwaka 2013 kabla ya uchaguzi.

Wagombea ni Army Sentimea na Said Nassoro (uenyekiti) wakati wanaoomba nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Juma Chaponda, Juma Mpuya na Tifika Kambimtoni.

Abdallah Mitole, Charles Ndagala na Hamis Kisiwa wanawania ukatibu mkuu, nafasi ya Mhazini inagombewa na Jovin Ndimbo. Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni Kamwaga Tambwe wakati nafasi ya uwakilishi wanawake yupo Isabela Kapera.

Wagombea wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Emmanuel Chaula na Samson Mkotya.

No comments:

Post a Comment