STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, February 12, 2013

YANGA KUSAKA POINTI ZA KUIACHA AZAM KWA LYON KESHO

Kikosi cha Yanga

Na Boniface Wambura
LIGI Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inamaliza raundi ya 16 kesho kwa mechi kati ya wenyeji African Lyon dhidi ya Yanga itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Martin Saanya kutoka Morogoro inakutanisha timu zenye mazingira tofauti. Wakati Yanga wakiwa ndiyo vinara wa ligi hiyo kwa pointi 33, African Lyon ambayo sasa inanolewa na Salum Bausi inakamata mkia ikiwa na pointi tisa tu.
Nayo Toto Africans iliyopo katika nafasi ya 12 itaikaribisha Polisi ya Morogoro kwenye Uwanja wa CCM Kirumba-Mwanza katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Jacob Adongo wa Musoma. Katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 20,000 utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting na Oljoro JKT.
Nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Mecky Maxime ambaye sasa ni kocha wa Mtibwa Sugar ataiongoza timu yake hiyo katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Turiani, Morogoro. Ni kwenye uwanja huo huo ambapo Mtibwa Sugar katika mechi yao iliyopita walichapwa mabao 4-1 na Azam.

No comments:

Post a Comment