STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, February 12, 2013

John Bocco 'Adebayor' aliyerejea toka kwenye majeruhi

TIMU ya soka ya Azam imesema ipo tayari kuwavaa Al Nasir Juba ya Sudan Kusini, hasa baada ya kurejea dimbani kwa washambuliaji wake waliokuwa majeruhi, Kipre Tchetche na John Bocco 'Adebayor'.
Azam na Al Nasir wanatarajiwa kuvaana Jumamosi kwenye uwanja wa Chamazi, likiwa ni pambano la awali la michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Afisa Habari wa Azam, Jaffer Idd Maganga aliiambia MICHARAZO jana kuwa, kikosi chao kimeshaingia kambini tangu jana asubuhi baada ya kutoka Morogoro ilipotoka kuiadhibu Mtibwa Sugar kwa kuilaza mabao 4-1 katika mechi ya Ligi Kuu.
Jaffer, alisema maandalizi waliyofanya wakati wakijiandaa na duru la pili la Ligi Kuu kwa kucheza michuano ya Mapinduzi na kusafiri katika nchi za DR Congo na Kenya yameiivisha Azam kimataifa.
Alisema kinachowapa faraja zaidi ni kupona kwa washambuliaji wao nyota, Kipre Tchetche ambaye Jumapili aliifungia Azam mabao mawili kati ya manne yaliyoizamisha Mtibwa, huku Bocco akiwa ameanza kufanya mazoezi mepesi na wenzake.
"Kwa kweli Azam tupo kamili gado kukabiliana na wageni wetu Al Nasir Juba, furaha zaidi ni kurejea kwa nyota wetu waliokuwa majeruhi kadhalika kikosi kina ari kubwa kwa ajili ya mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho," alisema Jaffer.
Aliongeza japo Bocco ameanza kujifua mazoezi na wenzake bado hawajajua kama ataweza kucheza katika pambano hilo,  kwa madai inategemea maamuzi ya kocha wao John Stewart Hall.
Azam inashiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza baada ya msimu uliopita kushika nafasi ya pili kwen ye Ligi Kuu Tanzania Bara nyuma ya Simba ambao watashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba wenyewe watashuka dimbani Jumapili kwenye uwanja wa Taifa, kuumana na Libolo ya Angola kabla ya kurudiana nao wiki mbili zijazo ugenini nchini Angola.
Kikosi cha Azam kitakachoshuka dimbani Jumamosi kuivaa Al Nasir Juba


No comments:

Post a Comment