STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, March 7, 2013

Golden Bush Veterani yampa shavu Mzee wa Kiminyio, kuivaa Baker Rangers


Kikosi cha Golden Bush Veterani katika picha ya pamoja

WAKALI wa soka la wazee jijini Dar e Salaam, Golden Bush Veterani imefanya mabadiliko katika benchi lake la ufundi ikijiandaa na pambano siku ya Jumamosi dhidi ya Baker Rangers.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa timu hiyo ambaye pia ni mlezi wa klabu hiyo, Onesmo Waziri 'Ticotico' uteuzi huo umefanywa wakijiandaa na mechi za sikukuu ya Pasaka.
Taarifa hiyo ya Ticotico imemtaja nyota wa zamani wa Majimaji, Simba na Taifa Stars, Madaraka Selemen kuwa ndiye kocha mkuu na msaidizi wake ni Herry Morris nyota za zamani wa Yanga.
"Tungependa kuwataarifu kwamba lie timu inayoogopwa sana hapa Dar es salaam imeanza Maandalizi rasmi kabisa ya game ya kumaliza ubishi Siku ya Pasaka na vibonde wetu Wahenga."taarifa ya Ticotico inasomeka hivyo kabla ya kuendelea; 
"Ili kujiweka sawa kabisa, timu yetu imefanya mabadiliko kidogo katika bench la ufundi ambapo kuanzia sasa Kocha Mkuu atakuwa Madaraka Seleman na Msaidizi wake ni Herry Morris ambaye atakuwa kocha mchezaji".
Taarifa hiyo iliongeza kwa kusema kuwa, Nahodha wa timu hiyo anasalia kuwa Yahya Issa akisaidiwa na Wazir Mahadhi na Nico Nyagawa.
Ticotico alidokeza kuwa timu hiyo imeanza mazoezi kabambe kabisa katika fukwe ya bahari na siku ya Jumamosi itashuka dimbani kuumana na Baker Rangers kabla ya timu kuingia kambini.

1 comment:

  1. Eeh mbona ni kama Tanzania Stars? Maana namuona Machuppa, Said Swedi, Shija Katina, Wazir Mahadhi, Nico Nyagawa, Steven Marashi? Ticotico ndiye yupi katika kikosi hicho maana nasikia kila mara akitajwa kama mkali.
    Mwanamicharazo

    ReplyDelete