STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, May 2, 2013

Redd's Miss Kigamboni 2013 kumekucha!

Somoe Ng'itu (wa pili toka kulia akiwa na wanahabari wenzake


MAZOEZI kwa ajili ya kujiandaa na shindano la kumsaka malkia wa kitongoji cha Kigamboni mwaka huu (Redd's Miss Kigamboni 2013) yataanza Jumatatu (Mei 6), Posta jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana, mratibu wa shindano hilo kutoka kampuni ya K& L Media Solutions, Somoe Ng'itu, alisema kuwa maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vyema na bado nafasi iko wazi kwa wasichana wote wenye sifa za kushiriki shindano hilo kutoka sehemu mbalimbali nchini.

Mratibu huyo alisema kwamba lengo la kuweka wazi na kuwahamasisha warembo ni kutaka kutoa nafasi kwa wasichana wengi zaidi kujiandikisha na hatimaye kupata mshindi atakayekiwakilisha vyema kitongoji hicho katika mashindano ya ngazi ya kanda yatakayofanyika mwezi ujao.

"Kila kitu kinaendelea vizuri na kamati ya maandalizi imewataka wadau wa sanaa ya urembo kujiandaa kuona mwaka huu shindano likiwa na ubora na mvuto zaidi," alisema Somoe.

Aliongeza kwamba fomu kwa ajili ya kushiriki shindano hilo zinapatikana bure na wanaotaka kushiriki wametakiwa kufika  Jumatatu, kwenye ukumbi wa Brake Point uliopo Posta ili kuanza mazoezi.

Mwaka jana, shindano hilo lilitoa mshindi katika kinyang'anyiro cha Kanda ya Temeke ambaye ni Edda Sylvester.

Edda alifanikiwa kushika nafasi ya tatu kwenye fainali za taifa huku mshindi wa taifa akiwa ni Brigitte Alfred.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment