STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, July 9, 2013

Maaskofu wawacharukia wanasiasa wanaotumia vibaya makanisa, msikiti

Askofu Mwamalanga
Na Suleiman Msuya
IKIWA ni siku chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete kuwataka viongozi na wanachama wa kisiasa kuacha kutumia nyumba za ibada kusakamana na kukashfiana viongozi wa dini wamemtaka kutumia nafasi yake kwa kuwataja wahusika kwani wanachochea uvunjifu wa amani.
Hayo yamebainishwa na Askofu  William Mwamalanga wa Kanisa la Kiinjili la Kipentakosti Tanzania pamoja na Mchungaji wa Kanisa la AGAPE Tanzania Onesmo Mwakyambo wakati wakizungumza na mwandishi wa habari hii.
Alisema ujumbe wa Rais ni muhimu hasa ukizingatia katika kipindi hiki ambacho kumejitokeza watu ambao wanaonekana kutumia nyumba za ibada kutoa misaada ambayo kwa upande mwingine kunatia shaka jamii ya Wanzania.
Mwamalanga alisema haipo sababu ya Rais kumumunya maneno kwani ni ukweli kuwa wahusika wakubwa wa mtindo huo wanatoka katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo ni vema wakakutana ili kukemea kichama zaidi.
“Mimi na baadhi ya viongozi wa dini na wananchi tunaamini kuwa Rais Kikwete amefanya jambo muhimu zaid katika kutatua hali ilivyo sasa kisiasa ila ni vema akaenda mbali zaidi kwa kuwaita hao wahusika na kuwakemea kichama kwani ni wanachama wa chama chake,” alisema
Askofu huyo alisema suala la baadhi ya viongozi wa kisiasa kutumia nyumba za ibada kwa kutoa misaada sio baya iwapo misaada hiyo ni safi ila akawataka kutambua kuwa ni vyema wakatubu iwapo wanatumia nafasi hiyo kujisafisha.
Mwamalanga alisema ni wazi kuwa Taifa linaweza kuingia katika hali sio sahihi iwapo haki za wananchi zitavunjwa kwani ni vigumu amani kuwepo katika eneo haki zinavunjwa.
Alisema watu baadhi wamefanikiwa kupoka haki za wananchi nje ya kanisa hali ambayo inaonyesha kuwa wanajipanga kuingia kuichukia haki iliyopo kanisani jambo ambalo amewataka viongozi wa kidini kupinga kwa nguvu zote.
Pia Askofu Mwamalanga alitoa wito kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiibuka na kujiita manabii kuwa waache kwani kufanya hivyo ni kinyume cha dini ya Kikristo.
Alisema kumekuwepo na uibukaji wa manabii wa uongo hasa katika mkoa wa Dar es Salaam jambo ambalo halipo katika maandiko na kuwataka viongozi wa dini kukemea hali hiyo kwani ni uzalilishaji wa dini.
Kwa upande wake Mchngaji Onesmo Mwakyambo ni vyema Serikali ikahakikisha kuwa amani inadumu kwani jamii ya Tanzania inatambua umuhimu wa kuwepo kwa amani ila kitendo cha viongozi kuwa sababu serikali itawajibika.
Alisema iwapo serikali itaangalia amani ikitoweka itambua kuwa athari zake ni kubwa kwani kwa muda mrefu jamii ya kitanzania imekuwa katika amani na upendo kama msingi wa maisha yao ya kila siku.
Mwakyambo alisema serikali inawajibika kuweka wazi mamabo yote ambayo yanalalamikiwa na wananchi kama moja ya njia ya kutatua matatizo hayo.
Aliwataka viongozi wa kidini kuacha kutumiwa kwani kufanya hivyo ni kukosea mungu jambo ambalo ni kinyume na mafundisho ya dini zao.

No comments:

Post a Comment