STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, July 9, 2013

Refa achinjwa Brazili ni baada ya kumchoma kisu mchezaji

Mwamuzi aliyeuwawa
MWAMUZI wa soka nchini Brazili, Otavio Jordao da silver (20) ameuwawa kikatili na kunyofolewa kichwa baada ya kumchoma kisu na kumuua mchezaji Josenir Dos Santos Abreu (30) uwanjani katika mechi ya kienyeji iliyofanyika June 30. Moranhao, Brazil.
Taarifa zinasema kuwa, refa huyo aliingia katika mzozo na mchezaji huyo baada ya kupuliza kipenga. baada ya kushindwana katika ubishi huo, refa alichukua kisu cha mfukoni na kumchoma mara nyingi na kusababisha kifo cha mchezaji huyo ambae alifia njiani akikimbizwa hospitali.
Baada ya tukio hilo watu walio na hasira na wanao aminika kuwa ndugu na marafiki wa mchezaji huyo, walimshambulia refa huyo, wakaanza kumpiga, wakamfunga na kumpiga na mawe kabla ya kumkata kichwa na kukitundika kwenye mti na baadae kukisimika katikati ya uwanja.
Mpaka sasa polisi wanamshikilia Luiz Moraes de souza (27) kwa tuhuma za mauaji hayo, ambae amekubali kumtukana refa huyo lakini amekanusha kumuua.

No comments:

Post a Comment