STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, July 9, 2013

TIC yafichua muarobaini wa tatizo la ajira nchini

Meneja Uhusiano wa TIC, Pendo Gongwe (Kati) akisisitiza jambo
Na Suleiman Msuya
ZAIDI ya ajira 174,412 zinatarajiwa kuzalishwa iwapo miradi 869 iliyosajiliwa Kituo cha Taifa cha Uwekezaji (TIC) itakamilika kwa wakati ulipangwa.
Hayo yamebainishwa na Meneja Mahusiano wa TIC Pendo Gondwe wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Alisema katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2012 TIC ilifanikiwa kusajili miradi 869 ambayo imegawanyika katika sekta mbalimbali ambayo inathamani ya dola za kimarekani shilingi milioni 11,420.
Gondwe alisema katika miradi hiyo 869 miradi 469 ni ya wazawa ambayo ni asilimi 54 na iliyobakia ni wawekezaji kutoka nje miradi 205 sawa na asilimia 23.5 na miradi ya ubia kati ya wageni na watanzania ni 195 sawa na asilimia 22.5  jambo ambalo ni la kujisifia kwa nchi.
Meneja huyo alisema sekta tano zimeongoza katika kuwekezwa ambazo ni sekta ya utalii miradi 144, usafirishaji 92, uzalishaji viwandani 86, majengo ya biashara 78 na kilimo miradi 28.
“ Ndugu zangu wanahabari napenda kutumia nafasi hii kuwataarifu kuwa miradi ya uwekezaji imeongezeka kwa ksi kubwa jambo ambalo tunaona na mwendelezo mzuri katika kukuza uchumi na ishara tosha ya kuonyesha kuwa nchi yetu ina usalama kwani hadi kufikia mwezi desemba mwaka jana miradi 869 imesajiliwa,” alisema.
Gondwe alisema jitihada za TIC ni kuhakikisha kuwa faida za uwekezaji katika uchumi wa Tanzania ikiwa ni kuweka mazingira rahisi kwa wawekezaji kuwa wanapata vibali vyote vinavyohitajika chini ya mfumo wa One Stop Shop.
Aidha alibainisha kuwa nchi kumi ambazo zinaongoza kwa uwekezaji hapo nchini kuwa ni Uingereza, China, India, Kenya Marekani, Uholanzi, Afrika Kusini, Canada, Ujerumani na Italia.
Naye Meneja Huduma kwa Wawekezaji Revocatus Arbogats alisema pamoja na ukweli kuwa miradi hiyo imesajiliwa lakini bado haijaanza kutoa matunda ya ajira kwani bado wawekezaji wako kwenye mchakato wa utekelezaji.
Alisema miradi hiyo itaanza kuonyesha matunda baada ya miaka mitatu ambapo watanzania wa kada mbalimbali wataanza kufaidika na ajira ambazo zitahusu uwekezaji husika.
Kuhusu wawekezaji kupendelea kuwekeza maeneo ambayo tayari wananchi wanaishi alisema kuwa hali hiyo inatokea mara chache baada ya mwekezaji kuonyesha kuwa eneo hilo linahusika na mradi.
Arbogats alisema pamoja na changamoto hizo TIC imekuwa ikijitahidi kutatua kwa kuhakikisha kuwa kila pande inaridhika na hatua ambazo zinachukuliwa.
Akizungumzia kuhusu sekta ya kilimo kuwa na wawekezaji wachache katika takwimu ambazo zimeanishwa Kaimu Meneja Utafiti wa TIC Nyoki Tibenda alisema sekta hiyo ni sekta muhimu ambayo inahitaji mitaji mikubwa bila kutarajia faida ya haraka.
Tibenda alisema TIC inaendelea kuwavutia wawekezaji ambao wapo tayari kuwekeza katika sekta hiyo ambapo alimtolea mfano mwekezaji aliyewekeza mkoani Morogoro Kilombero katika kilimo cha mpungu kuwa ameonyesha mafanikio makubwa.

No comments:

Post a Comment